WATUMISHI wa afya 21 kutoka kitengo cha kuhudumia watu waliopatwa na majeraha katika ajali  (trauma unit) cha Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka kwa wataalam wa matibabu kutoka Israeli.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dr Alphonse Chandika, amebainisha kuwa mafunzo hayo ya siku sita yaliandaliwa kwa ajili ya kuwapatia maarifa wataalamu hao ili kuendesha kitengo hicho kiufanisi.

“Mafunzo ya kuwajengea uwezo ni muhimu ili kuwawezesha wataalamu wa tiba kuendesha ahiki kipya kiufanisi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali wakati akizungumzia juu ya ujio wa Mkuu wa Mashav, Balozi Gil Haskel.

Mashav ni Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa ambalo limewezesha kuanzishwa kwa kitengo hicho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa baada ya makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Israeli miaka miwili iliyopita.

Dk Chandika alitoa shukrani kwa Israeli kwa msaada wa kitengo hicho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, akibainisha kuwa kitengo cha trauma kitasaidia kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo ya umma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali alisema uzinduzi rasmi wa kitengo hiko utakuwa kati ya Juni na Julai mwaka huu, akisema kiengo hicho kitatoa huduma kwa watu ambao wamepatwa na ajali na majeruhi ya kudumu kutoka kwa majeraha makubwa ya mgongo na majeraha madogo ya mifupa na hali.

Kitengo hiki kinatarajiwa kutoa huduma ambazo zinajumuisha huduma maalum ya matibabu na uuguzi, dawa za dharura, upasuaji, huduma za msingi, upasuaji wa neva, upasuaji wa meno.

Kwa mujibu wa Balozi Haskel, ziara yake ilikuwa na lengo la ziara yake ni kukagua kitengo hicho ambacho kuanzishwa kwake kulifadhiliwa na Mashav.

“Hii inaonyesha uhusiano mkubwa kati ya Israeli na Tanzania. Tutaendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, “alisema.

Watumishi wa afya wa kitengo kipya cha kuhudumia watu waliopatwa na majeraha katika ajali (Trauma Unit) cha BMH katika picha ya pamoja na Balozi Gil Haskel na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Alphonce Chandika baada ya kumaliza mafunzo.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano cha BMH

CategoryNews

Copyright © 2018 - Benjamin Mkapa Hospital All rights reserved

Privacy Policy    |   Disclaimer   |    Sitemap