SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani kwa mwaka 2022 ni: Kusogeza huduma za Homa ya Ini jirani na Jamii (“Bringing Hepatitis care closer to Communities”). Kauli mbiu hii inatulazimu kusogeza huduma kwa Jamii ili kudhibiti ugonjwa huu nchini na hatimaye kuweza kuutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030.