BMH, KUWA HOSPITALI YA TAIFA
BMH, KUWA HOSPITALI YA TAIFA

BENJAMIN MKAPA KUWA HOSPITALI YA PILI YA TAIFA

 

Dodoma Leo Julai 1,

 

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) amehaidi kuwa kufikia Julai 2025 atahakikisha hospitali ya Benjamin Mkapa inakuwa Hospitali ya pili ya Taifa nchini  ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya  kwa haraka.

 

Mshemiwa Waziri ameyasema hayo leo alipofika katika Hospitali hiyo kuzindua mtambo wa kuzalisha Hewa Tiba ya Oksijeni utakaopunguza mahitaji ya hewa tiba hiyo kwa hospitali zilizo katika mikoa ya Kanda ya kati.

 

“Nimekusudia itakapofika julai 2025 au kabla, Benjamin Mkapa Hospital ipate hadhi ya Hospitali ya Taifa” Alisema na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa hospitali hiyo kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.

 

Akiwa hospitalini hapo pamoja na Uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni, Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu amezindua kitabu cha Mwongozo wa utoaji  dawa cha Hospitali ya Benjamin Mkapa kinacholenga kukuza matumizi sahihi ya  wagonjwa wanaopatiwa matibabu.

 

Katika taarifa yake Dkt. Alphonce Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo aliainisha mipango ya Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na, Kujenga kituo cha Matibabu ya Moyo,  Kituo cha Matibabu ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Uti wa Mgongo, Pamoja na maendeleo ya Ujenzi wa kituo cha Matibabu ya Saratani kwa njia ya Mionzi.

 

 

 

 

 

 

Dondoo za Afya na Habari
Kula Mlo Kamili
Kula Mlo Kamili

Eat a combination of different foods, including fruit, vegetables, legumes, nuts and whole grains. A...

  View more
Usivute Sigara
Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mapafu yako, uvutaji wa sigara unaweza sababisha matatizo ya...

  View more
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta

Fats consumed should be less than 30% of your total energy intake. This will help prevent unhealthy...

  View more
Kuendesha Gari.
Kuendesha Gari.

Unashauriwa kutokuendesha gari kila siku na wakati mwingine unatakiwa kutembea walau miguu yako na m...

  View more
Epuka ulevi wa Pombe
Epuka ulevi wa Pombe

There is no safe level for drinking alcohol. Consuming alcohol can lead to health problems such...

  View more