Mwanzo / Kurasa / Sehemu ya Upasuaji wa Macho

Sehemu ya Upasuaji wa Macho

Published on August 13, 2022

Idara ya Magonjwa ya Macho ilianza kutoa huduma kwa wananchi wenye matatizo ya macho mnamo oktoba, 2015 kwa kutoa huduma za kliniki pekee.

Kwa wakati huo 2015, Idara ya Magonjwa ya macho iliendeshwa na Muuguzi mmoja wa macho, pamoja na daktari bingwa wa macho. 

Baadae, idara ya Magonjwa ya macho iliongeza muuguzi msaidizi wa macho na kuiwezesha kufanya huduma-mkoba iliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali, huduma hiyo ilisababisha idara ya macho kufahamika miongoni mwa wananchi.

Baada ya huduma-mkoba kuitambulisha Idara ya Magonjwa ya macho, ikiwa ni pamoja na kupata ufadhili wa vifaa vichache kutoka kwa wadau  hao, Idara iliweza kuongeza huduma na kuanza kufanya upasuji mdogo.

Mnamo mwaka 2018, Idara ya Magonjwa ya Macho ilipata Madaktari wengine wawili, hivyo kufanya idadi ya watumishi katika idara hiyo kuwa watano (05).

Baada ongezeko la watumishi idara ilifanikiwa pia kupata Hadubini yenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibu (operating microscope) inayotumika hadi sasa.

Kwa bahati nzuri, shirika lingine lisilokuwa la kiserikali (NGO) lijulikanalo kama KCCO liliamua kufadhili huduma-mkoba kwa wagojwa wenye mtoto wa jicho, na kwa sababu hiyo, walinunua Hadubini nyingine yenye uwezo wa kuchunguza na kutibu.

Kuanzia mwaka 2019, Idara ya magonjwa ya macho imekuwa ikikua siku hadi siku, kufikia idadi ya manesi wawili wa macho, Madaktari wa macho wawili, Muuguzi msaidizi mmoja, Meneja wa Huduma Mkoba mmoja, na mtoa huduma za jamii mmoja.