Mwanzo / Kurasa / Magonjwa ya Maskio, Pua na Koo

Magonjwa ya Maskio, Pua na Koo

Published on August 12, 2022

Idara ya Masikio, Pua na Koo, ilianza kutoka huduma mapema  Oktoba, 2015 ikiwa na Daktari Bingw ammoja wa kuazimwa kutoka katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa Dodoma kwa kuona Wagonjwa wa nje, na alikuwa akihudumia Mgonjwa mmoja hadi wanne, na wote walikuwa wagonjwa wa nje ( outpatient).

Idara ya Masikio, Pua na Koo, ilipata Daktari wake mwaka 2017, kwa maana ya mwajiriwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, jambo lilichagiza kuongezwa kwa huduma za upasuaji wa Masikio, Pua na Koo huduma ambazo zilizalisha huduma za (inpatient).

Idara ya Masikio, Pua na Koo, ilipata Vifaa tiba vya kisasa aina ya ‘Endoscopic instruments’ vifaa hivyo, viliwezesha kuboresha huduma katika Idara ya ENT, ambapo ilianza kutoa huduma za Functional Endoscopic Sinus (FESS), Husuma za uchunguzi kwa kutumia vifaa hivyo, Upimaji wa usikivu, pamoja na kutoa vifaa vya kusaidia usikivu (hearing aids).

Hadi kufikia Januari 2022, Idara ya Masikio, Pua na Koo, inao watumishi kumi, ikiwa ni pamoja na madaktri bingwa, Madaktari wakazi, Madktari, Wauguzi na Wahudumu, kwa wastani wanaona kati ya wagonjwa 40-60 kwa siku na hufanya upasuaji kwa wagonjwa kati ya 15-20 kila wiki