TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGONJWA USIOFAHAMIKA MKOA WA LINDI.
Ndugu Wananchi, Tarehe 7/7/2022, Wizara ya Afya ilipokea taarifa toka kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Lindi kuwa katika Halmashauri ya Ruangwa kumekuwepo na Ugonjwa usio wa kawaida kutoka Kituo cha Afya Mbekenyera, ambapo Ndani ya siku 3 (tarehe 5 na 7 July 2022) walipokea Wagonjwa 2 katika kituo hicho wakiwa na dalili za homa, kuvuja damu (hususan puani), kichwa kuuma na mwili kuchoka sana. Wizara iliunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na Majanga, Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Utafiti (NIMR), Chuo kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliungana na timu ya Mkoa ikihusisha pia Idara ya Mifungo.