Elimu na Mada Tiba
Kurugenzi ya Mafunzo na Utafiti imegawanyika katika sehemu mbili;
1. Uratibu wa Mafunzo na huduma mkoba, ambayo ina majukumu yafuatayo
-Kuratibu mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
-Kuratibu programu za huduma mkoba
-Kuratibu programu za mafunzo maalumu kama vile kambi maalumu
-Kuwezesha programu fupi za mafunzo kama vile Cheti cha Umahiri katika masuala ya usingizi (Anesthesia) ambayo ni kozi inayoendelea
Jukumu jingine ni
-Kuratibu mafunzo endelevu ya elimu ya matibabu (CME) vya Hospitali
2. Sehemu ya Utafiti
-Kuratibu shughuli za utafiti zinazofanyika BMH
-Kuratibu na kutoa kibali cha utafiti wa nje uliofanywa BMH
-Kuomba fedha zinazohusiana na utafiti
-Kuandaa na kuhuisha sera, mikakati na miongozo inayohusiana na utafiti BMH
- Usimamizi wa miradi ya utafiti
-Kuendeleza miundombinu ya utafiti
-Kusaidia na kusimamia wafanyakazi wa Hospitali juu ya kufanya utafiti na uchapishaji
-Kuanzisha na kudumisha maadili ya utafiti
-Kuandaa mwongozo wa ushauri
- Kuratibu Bodi ya Ukaguzi wa Taasisi (IRB) kwa ajili ya utafiti katika BMH