Mwanzo / Huduma Zetu / ALAMEDA WAITEMBELEA BMH

ALAMEDA WAITEMBELEA BMH

Published on October 20, 2022

Article cover image

Dodoma Oktoba 20, 2022.

Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kushirikiana na Hospital ya Alameda ya nchini Misri ili kuendelea kuboresha na kukuza viwango vya utoaji huduma za kingwa na Ubingwa bobezi kwa kutumia maarifa na teknolojia mpya za tiba.

Hayo yamebainishwa leo mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Alameda alipo itembela Hospitali ya Benjamin Mkapa kujionea hali ya Miundombinu kabla ya kuanza kutekeleza mashirikiano hayo. 

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Afya Dkt. Waryoba Nyakuwa, Wizara ya Afya imeingia Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Hospitali zote za Kibingwa nchini kushirikiana na Alameda ili kujengeana uwezo katika maeneo mbalimbali ujuzi na teknolojia za  huduma za kibingwa na Ubingwa bobezi.

“Mashirikiano haya yanalenga kubadilishana ujuzi wa kutoa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi, na pia yanaangazia mabadiliashano ya teknolojia za matibabu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa huduma bora zinazopatikana jirani na mazingira yao” Alisema Dkt. Nyakuwa.

Akitoa neno la utangulizi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Kessy Shija, amewahakikishia Alameda kuwa wapo tayari kushirikiana kwa kuwa Hospitali hiyo inawataalamu waliyobobea na vifaa tiba vya kisasa kuwezesha huduma za kiwango cha juu cha ubora.

“Kuna maeneo ya Huduma za matibabu ya Moyo, Figo, Saratani, Ubongo na Mishipa ya Fahamu, Mfumo wa Mkojo na Mifupa, yote haya yanahitaji kukuza ujuzi kuendana na kasi ya mabadililiko ya teknolojia ya tiba, hivyo ushirikiano huu utakuwa wenye manufaa kwetu na kwa wananchi wetu” Alieleza Dkt. Kessy.

 Kwa upande wake Dkt. Amira Hamounda, Mkurugenzi wa Alameda anayeshughulikia maendeleo ya biashara za kimataifa ameridhishwa na miundombinu pamoja na vifaa tiba alivyoviona Hospitalini hapo, na kwamba wanatarajia kuona maeno ya mashirikiano baina yao na Hospitali ya Benjamin Mkapa.

“Tumebobea katika Matibabu ya Moyo, Mfumo Fahamu, Kansa, Sayansi Figo na Mifupa, hivyo tuona maeneo gani tutashirikiana” Alisema Dkt. Amira

 Ndani ya miaka saba tangu Hospitali ya Benjamin Mkapa ilipoanza kutoa huduma za Afya, imekuwa suluhisho muhimu kwa magojwa yasiyoambukiza kama vile Magojwa ya Moyo, Figo, Saratani, Selimundu na Mifumo wa Fahamu na Ubongo kama ilivyokusudiwa wakati ikianzishwa. Ushirikiono baina yake na Alameda utaongeza chachu zaidi ili wananchi wengi wapate suluhu za maradhi yanayowakabili.