Mwanzo / Huduma Zetu / BMH KUJENGEWA KITUO CHA UMAHIRI CHA UPANDIKIZAJI ULOTO EAC

BMH KUJENGEWA KITUO CHA UMAHIRI CHA UPANDIKIZAJI ULOTO EAC

Published on May 14, 2024

Article cover image

Hospitali Benjamin Mkapa (BMH) itajengewa Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto cha Jumuiya ya Afrika Mashariki  (EAC), kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu.

Wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2024-2025, Waziri Mhe. Ummy, amesema BMH imechaguliwa na EAC kwa kuwa ni Hospitali pekee katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kutoa huduma hii muhimu afya.

"Napenda kumpongeza Dkt. Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa na timu yake," amesema Mhe. Waziri. 

Upandikizaji uloto ni matibabu yanayotolewa na BMH kutibu siko seli. Huduma hii imezinduliwa Mei, 2023.

Mpaka sasa, watoto 10 waliokuwa na siko seli wameishapandikizwa uloto  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), huku vipimo vikiwa vimethibitisha kuwa watoto wanne wa kwanza waliotimiza mwaka mmoja toka kupata kupata matibabu hiyo wamepona ugonjwa huo.