BMH, KUWA HOSPITALI YA TAIFA
BENJAMIN MKAPA KUWA HOSPITALI YA PILI YA TAIFA
Dodoma Leo Julai 1,
Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) amehaidi kuwa kufikia Julai 2025 atahakikisha hospitali ya Benjamin Mkapa inakuwa Hospitali ya pili ya Taifa nchini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa haraka.
Mshemiwa Waziri ameyasema hayo leo alipofika katika Hospitali hiyo kuzindua mtambo wa kuzalisha Hewa Tiba ya Oksijeni utakaopunguza mahitaji ya hewa tiba hiyo kwa hospitali zilizo katika mikoa ya Kanda ya kati.
“Nimekusudia itakapofika julai 2025 au kabla, Benjamin Mkapa Hospital ipate hadhi ya Hospitali ya Taifa” Alisema na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa hospitali hiyo kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.
Akiwa hospitalini hapo pamoja na Uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni, Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu amezindua kitabu cha Mwongozo wa utoaji dawa cha Hospitali ya Benjamin Mkapa kinacholenga kukuza matumizi sahihi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu.
Katika taarifa yake Dkt. Alphonce Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo aliainisha mipango ya Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na, Kujenga kituo cha Matibabu ya Moyo, Kituo cha Matibabu ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Uti wa Mgongo, Pamoja na maendeleo ya Ujenzi wa kituo cha Matibabu ya Saratani kwa njia ya Mionzi.