Mwanzo / Huduma Zetu / WATOTO 72 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO, UPASUAJI MKUBWA NA UPASUAJI MDOGO

WATOTO 72 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO, UPASUAJI MKUBWA NA UPASUAJI MDOGO

Published on February 14, 2023

Article cover image

Dodoma; Februari 10 2023.

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la The Childrens Heart Charity Association kutoka nchini Kuwait wamefanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa Watoto iliyohusisha uchunguzi wa kibingwa, matibabu na upasuaji.

Katika kambi hiyo Watoto 66 walifanyiwa uchunguzi, 3 upasuaji mkubwa wa kuziba matundu katika moyo huku 5 wakifanyiwa upasuaji mdogo wa kuziba matundu katika mirija ya damu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa Hospitali imeingia makubaliano na shirika hili katika kutoa matibabu ya moyo kwa Watoto kwani kwa mwaka Watoto 3,400 huzaliwa na matizo ya moyo nchini.  

“Kutokana na tatizo hili kuwa kubwa nchini, BMH kushirikiana na Childrens Heart Charity Association watafanya uchunguzi wa bure wa magonjwa ya moyo kwa Watoto 100 katika kila kambi itakayofanyika ndani ya miaka mitatu,” amesema dkt. Chandika.

Dkt. Chandika ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Hospitali vifaa vya kisasa na kurahisisha ushirikiano na shirika hilo kutoka Kuwait.

Kiongozi wa Shirika la Childrens Heart Charity Association Dkt. Faisal Al-Saeedi ameahidi kuwajengea wataalamu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa uwezo Pamoja na kutoka vifaa vya matibabu.

“Naishukuru BMH kwa mapokezi mazuri na ushirikiano wao kati kipindi chote cha kambi na naahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika huduma za matibabu ya moyo nchini,” aliongeza Dkt. Al-Saeedi.