Mwanzo / Huduma Zetu / Dkt. CHANDIKA: BIMA YA AFYA KWA WOTE ITAONGEZA WIGO WA HUDUMA

Dkt. CHANDIKA: BIMA YA AFYA KWA WOTE ITAONGEZA WIGO WA HUDUMA

Published on January 23, 2023

Article cover image

Januari 23, 2023 Dodoma 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)-Dodoma, Dkt Alphonce Chandika amesema kuwa Bima ya Afya kwa Wote itaongeza wigo wa huduma na kuwafaidisha wananchi waliyokuwa hawamudu gharama za uchunguzi na matibabu.

Dkt. Chandika aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akitoa taarifa katika kikao cha Mkoa wa Dodoma kuhusu mafanikio ya serikali ya wamu ya sita, kilichowahusisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata hadi Mkoa na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa viongozi hao kushiriki kutoa elimu ya faida Bima ya Afya kwa Wote.

“Bima ya Afya kwa Wote itaongeza wigo wa huduma kwa wananchi, hasa wale waliyokuwa wanashindwa kumudu gharama za uchunguzi na matibabu”Alisisitiza Dkt. Chandika.

Katika hatua nyingine Dkt. Chandika aliishukuru Serikali kwa kusudio lake la kuleta  Bima ya Afya kwa Wote kwa kuwa itaondoa manungúniko na mapungufu mbalimbali yaliyochangiwa na baadhi ya wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Aidha katika kikao hicho, Dkt. Chandika aliwaomba viongozi mbalimbali wakiwe wa dini, wa kiasiasa na wa serikali waliohudhuria kikao hicho kuwahamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote itakapoanza, kwa kufanya hivyo, huduma za Afya zitaboreshwa zaidi utawasaidia wananchi kuwa na uhakika wa matibabu wakati wote.