Mwanzo / Huduma Zetu / KAMATI YA BUNGE YA AFYA YA NAMIBIA YAITEMBELEA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA.

KAMATI YA BUNGE YA AFYA YA NAMIBIA YAITEMBELEA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA.

Published on June 14, 2023

Article cover image

Kamati ya kudumu ya masuala ya usawa wa jinsia, maendeleo ya jamii na ustawi wa familia kutoka Bunge la Namibia leo wamefanya ziara katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) lengo likiwa ni kujifunza jinsi BMH inavyotoa Huduma kwa wananchi.

Kamati hiyo iliyopokelewa na Mhe. Ummy Mwalimu (Mb)Waziri wa Afya  pamoja na menejimenti ya Hospitali ililenga kujifunza namna Huduma za afya zinavyotolewa BMH na Tanzania kwa ujumla.

 Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) Waziri wa Afya aliwaelezea namna Tanzania inavyotoa Huduma ya uchujaji damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na hatua nchi iliyopiga katika kupambana na magonjwa wa figo.

“Kwa upande wa Hospitali ya Benjamin Mkapa walianza kutoa Huduma za kuchuja damu na kupandikiza figo mwaka 2018 na mpaka sasa wana mashine 30 za kuchuja damu” alisema Mhe. Ummy

Lengo la serikali ni kuhakikisha kila Hospitali ya rufaa ya mkoa ina mashine za kuchuja damu na mpaka sasa Hospitali 10 kati ya 28 zimepatiwa mashine hizo na huduma inaendelea aliongeza Mhe. Ummy

“Malengo yetu ya baadae ni huduma ipatikane mpaka kwenye Hospitali za wilaya,” alieleza Mhe. Ummy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika aliwaelezea wabunge hao huduma zinazotolewa na BMH kwa ujumla.

“Katika Hospitali yetu ya Benjamin Mkapa tunatoa Huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya figo, Watoto, mifupa, magonjwa ya wanawake, tunatoa Huduma za moyo na huduma ya matibabu ya Moyo kwakutumia mtambo wa CathLab na pia tunatoa Huduma za Upasuaji,” alieleza Dkt. Chandika.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya masuala ya usawa wa jinsia, maendeleo ya jamii na ustawi wa familia kutoka Bunge la Namibia Mhe. Gotthard Kasato amemshukuru  Mhe. Ummy Mwalimu (Mb)Waziri wa Afya kwa kutenga muda wake na kukutanao nao.

“Asante sana Mhe. Waziri wa Afya kwa kutenga muda wako na kukutana na sisi kwani sio jambo la kawaida,” Alieleza Ndg. Gotthard.

Tumeridhishwa na namna Hospitali ya Benjamin Mkapa inavyotoa Huduma na tumefurahia kuona maendeleo makubwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa aliongeza Ndg. Gotthard.