Mwanzo / Huduma Zetu / KAMBI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO INAENDELEA

KAMBI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO INAENDELEA

Published on March 22, 2023

Article cover image

Madaktari bingwa wa Moyo wa Hospitali ya Benjamini Mkapa na Chuo Kikuu Dodoma UDOM, kwa kushirikiana na wenzao kutoka shirikia lisilo la kiserikali la One New Heart Tanzania na For the Heart and Soul kutoka nchini Marekani leo wameanza kambi maalumu ya uchunguzi na Matiababu ya Moyo kwa Watoto kuanzia Miaka 0-17.

Kwa mujibu wa Dkt. Rehema Yona, ambaye ni daktari bingwa wa Watoto amesema kuwa kambi hiyo inawalenga Watoto wenye viashiria vya magonjwa ya Moyo ikiwemo, kutoongezeka uzito, kupumua kwa shida, kuchoka, kikohozi cha mara kwa mara, mtoto kushindwa kunyonya na kutokwa jasho jingi wakati wa kunyonya Pamoja na kushindwa kuhimili mazoezi.

“natoa wito kwa wazazi wenzangu wenye Watoto waoonesha viashirika kama hivyo kuwaleta Watoto wao hapa Benjamin Mkapa, tunawafanyia uchunguzi bila malipo, wenye kuhitaji tiba wanazipata” Alisema Dkt. Rehema

Baadhi ya wazazi waliyofika hospitalini hapo kupeleka Watoto wao kuchunguzwa na kupatiwa matibabu wameridhishwa na kufurahishwa na huduma hizo bila malipo.

Rechel Levison mkazi wa Kibaha-Pwani aliyefika Hospitali hapo kumpeleka binti yake (Umri 5), anayesumbuliwa na tatizo la kupumua amefurahishwa na huduma alizozipata.

“nimepokelewa vizuri, nimepata huduma vizuri naupongeza uongozi wa Benjamin Mkapa kwa kuandaa kambi ya matibabu ya Moyo ya bure kwa Watoto” Alisema Bi. Rechel.

John Mwilongo Mkazi wa Nkuhungu-Dodoma, aliyefika Benjamin Mkapa akiwa na Watoto wake wawili (umri 5 na 2) mmoja akiwa na tatizo la kupumua mwingine aliambana ili kutumia fursa hiyo kufanyiwa uchunguzi kwa kuwa unanyika bure.

“Kambi ni fursa kwa watu wengi hasa wasiyojiweza kwa kuwa inatoa fursa kwao kupata huduma za kibingwa bure, hivyo naupongeza uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuleta kambi hii” Aliema Bwana Mwilongo.

Kambi hiyo itaendelea hadi tatu mfululizo hadi Machi 24, 2023 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 09:30 mchana, hivyo wazazi mnahimizwa kuendelea kuwaleta Watoto wahudumiwe kwa huduma za uchunguzi na matibabu ya Moyo kwa Watoto yanatolewa bure kwenye kambi hiyo.