Mwanzo / Huduma Zetu / MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA UPANDIKIZAJI FIGO BMH

MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA UPANDIKIZAJI FIGO BMH

Published on March 17, 2023

Article cover image

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) leo imetimiza miaka mitano toka ilipoanzisha huduma hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika, wagonjwa 33 wamekwishapandikizwa figo mpaka sasa katika hospitali hii ya umma.

"Kuanzishishwa kwa huduma hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa imesaidia Serikali kuokoa fedha za kigeni zilizotumika kwa rufaa nje ya nchi," alisena Mkurugenzi Mtendaji.

BMH ilikuwa hospitali ya pili nchini Tanzania kuanzisha huduma hiyo miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa Dkt. Chandika, BMH ilianzisha huduma kwa usaidizi kutoka Shirika la Tokushukai la nchini Japan.

Lakini, Dkt Chandika, anaongeza kuwa mwaka 2021, BMH walianza kupandikiza figo kwa kutumia wataalamu wake wazawa.