Mwanzo / Huduma Zetu / MENEJIMENTI YA BMH KUWATENGENEZEA MAZINGIRA MAZURI MADAKTARI KUTOA HUDUMA BORA

MENEJIMENTI YA BMH KUWATENGENEZEA MAZINGIRA MAZURI MADAKTARI KUTOA HUDUMA BORA

Published on July 02, 2024

Article cover image

Na Carine Abraham Senguji, Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof Abel Makubi, akiambatana na Menejimeti amewataka madakatari kuendelea kuboresha huduma za tiba kwa Wananchi huku Hospitali ikiwatengenezea mazingira bora zaidi ya kutekeleza majukumu yao .

Prof. Makubi ameeleza moja ya mihimili  mikuu ya huduma bora ni daktari : hivyo daktari ana kila sababu ya kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya kazi, ikiwemo hata muda za ziada .

"Daktari ndiye anakaa na mgonjwa na kuongea naye hivyo ni lazima mazingira ya kutekeleza majukumu yake yawe rafiki ili mgonjwa apate huduma anazostahili" aliongeza Prof. Makubi

Prof. Makubi ameendelea kuwataka Madaktari kumpatia mgonjwa matibabu yote anayo stahili

"Mgonjwa anapokuja Hospitali ya Benjamin Mkapa ni matumaini yake amekuja kupata matibabu yote na ndiyo maana akirudi nyumbani anasema nimeonwa kila kitu hawaoni kitu, hivyo nilazima tujitofatishe na Hospitali nyingine katika kuwahudumia wagonjwa kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa" alisema Prof Makubi 

"Madaktari hamjakosea kusomea hii kazi nawaomba mjiamini mpo sehemu sahihi ya kurejesha afya wa Wananchi na pia bado taaluma hii inawapatia stahili zenu halali ; alisema Prof Makubi.