Mwanzo / Huduma Zetu / MENEJIMENTI YA BMH YASHIRIKI MKUTANO WA TATHMINI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA PEPMIS/PIPMIS

MENEJIMENTI YA BMH YASHIRIKI MKUTANO WA TATHMINI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA PEPMIS/PIPMIS

Published on May 17, 2024

Article cover image

Menejimenti ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imeshiriki mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi na Taasisi (PEPMIS/PIPMIS) . Mkutano huu muhimu umeitishwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawakabora kwa kushirikiana na Wizara ya Afya mahsusi kwa viongozi wa Wizara na Taasisi zake kujenga uelewa wa pamoja wa mfumo na kutafuta Ufumbuzi. 

Msimamizi Mkuu wa Mafunzo hayo Bi. Felister E. Shuli ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma , alisisitiza kuwa Serikali imeamua kutumia Mifumo ya TEHAMA kupima utendaji kazi na haitarudi nyuma Hivyo kila mtumishi wa Umma ni starti aweke nia ya kutekeleza. 

Akiongoza viongozi wa Menejimenti ya BMH Bi. Prisca Lwangili ameeleza mfumo wa  PEPMIS kuwa nyenzo bora katika ufuatiliaji wa utendaji kazi na ameahidi kuendelea kuutumia ipasavyo.

"Tuna kila sababu ya kuwa mstari wa mbele ili kufikia azma ya Serikali kuutumia mfumo huu kwa usahihi ili kuongeza ufanisi wa upimaji wa  utendaji kazi katika Taasisi na kuimarisha huduma" alisema Bi. Prisca.