Mwanzo / Huduma Zetu / MIAKA 7 YA BMH: MKURUGENZI AELIMISHA BIMA YA AFYA KWA WOTE

MIAKA 7 YA BMH: MKURUGENZI AELIMISHA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Published on October 13, 2022

Article cover image

Dodoma Oktoba 13, 2022

Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo Oktoba 13, imetimiza miaka saba tangu ilipoanza kutoa huduma za Afya Oktoba 13, 2015.

Mkurugenzi Mtendaji Dkt, Alphonce Chandika amewajengea uwelewa juu ya Msuada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote wananchi waliyofika kupata huduma, ambapo mesema  lengo la Mswada huo ni kuhakikisha, kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata matibabu bila hofu.

“Ndugu zangu baadhi yenu mnakuja hapa mara kwa mara kupata huduma, mnafahamu ugonjwa haubishi hodi, bila kuwa na BIMA kuna wenzetu hulazimika kuuza hata viwanja au nyumba wagharamie matibabu” Alidokeza, Dkt. Chandika.

Aidha, alifafanua kuwa mantiki ya Mswaada wa BIMA ya Afya kwa wote ni kuhakikisha kuwa, watu wengi wanachangia gharama za matibabu kabla hawajafikwa na maradhi ili kutunisha mfuko hatimae mtu akiugua asikutane na changamoto yoyote ya kukosa huduma kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu.

“Msingi wa BIMA ya Afya kwa wote, ni suala la upendo zaidi, na baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tunaeadhimisha  siku yake kesho alitufundisha kupendana, hivyo tunapochangia wengi, wakaugua baadhi tunakuwa tumewasaidia” Alifafanua Dkt. Chandika.

Vile vile, alieleza kuwa mapendekezo ya Mswada huo ni kwa kaya moja kuchangia Shilingi 340,000 na kunufaisha wanafamilia sita, huku mtu mmoja akitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 84,000 ili kupata huduma za Afya kwa mwaka mzima.

“Nasisitiza kuwa serikali haina lengo la kumlazimisha mtu kuchangi, bali itaweka mazingira rafiki yatakayomsukuma kila mmoja kuona umuhimu wa kuchangia, na kwa kutumia mifumo ya TASAF na Ustawi wa jamii itawatambua wasiyojiweza na kuwatengenezea mfumo wa kupata matibabu bila usumbufu” Alisema Dkt. Chandika.

Shamrashamra za kutimiza miaka hiyo saba zimeanza saa mbili asubuhi ya leo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika kushiriki kutoa huduma za msingi kwa wagonjwa, aliwapokea, kuzungumza nao na kuwasaidia waliyohitaji kutembea kwa msaada wa kiti maalumu (Wheelchair). 

Kisha aliwashukuru wananchi waliyofika Hospitalini hapo kwa kutoa mchango wao wa maoni, ambayo hupokewa na kufanyiwa kazi kwa wakati na ndiyo umekuwa msingi wa maboresho mbalimbali ya huduma katika Hospitali hiyo kiasi cha kuifanya kutambuliwa kama kinara kwa Utoaji wa huduma bora za Afya kwa Hospitali zote nchini.

Kwa asubuhi ya leo, sherehe hizo ziliahanikizwa na ukataji wa keki  maalumu ya miaka saba ya huduma katika Hospitali hiyo, ambayo ilikatwa kwa ushirikiano wa Mteja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Baadaye alielekea katika wodi ya watoto wachanga na kutoa zawadi mabalimbali kwa watoto hao kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.

Na. Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano BMH.