Mkurugenzi Mtendaji BMH akutana na Mabalozi
Mkurugenzi Mtendaji BMH akutana na Mabalozi

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika leo amekutana na mabalozi wa Tanzania waliopo Mashariki ya kati,Ulaya na Amerika, Asia pamoja na Australasia kwa dhumuni la kuwaeleza mafanikio yaliyo letwa na Serikali katika sekta ya afya.

"Hospitali ya Benjamin Mkapa ni Hospitali ya Serikali inayo wahudumia wananchi wote kwa kiwango kinacho stahili"alisema Dkt.Chandika 

Dkt. Chandika aliongeza kuwa "Serikali imewekeza pesa nyingi kwa kuweka majengo mazuri, vifaa tiba vya kisasa na rasilimali watu, hivyo nasi tunatoa huduma kwa viwango hivyo hivyo, tokea Hospitali ianzishwe mahusiano baina ya Hospitali na nchi za nje yamekuwa yakiimarika siku kwa siku"

Kwaupande wake Mhe. Balozi Dkt Asha Rose Migiro ameipongeza Hospitali kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma zinazoendana na teknolojia ya sasa tena kwakuzingatia huduma kwa mteja. 

"Ukifika Hospitali ya Benjamin Mkapa huitaji kujitambulisha ili upate huduma nzuri maana utahudumiwa kwa kiwango kizuri pasipo kujali wadhifa wako kwakweli mnastahili pongezi kubwa, endeleeni na moyo huo wa kuwahudumia wananchi pasipo kubagua" alisema Dr Migiro, ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Aidha Mhe. Balozi Swaiba Mndeme ameeleza nimuhimu kuzisaidia Taasisi zetu hususani Hospitali  "Tunaposaidia hizi Hospitali tunakuwa tumewafikia wananchi moja kwa moja nasi shabaha yetu iwe ni kuwasidia wananchi kwa kuiunganisha BMH na wataalamu walipo kwenye nchi tulizopo"alisema Balozi Swahiba.

Hospitali ya Benjamin Mkapa ilizinduliwa Tarehe 13/10/2015 tokea izinduliwe imekuwa ikikuwa kwa kasi kubwa huku ikitoa huduma zake kwa ubunifu wa hali ya juu.

Dondoo za Afya na Habari
Kula Mlo Kamili
Kula Mlo Kamili

Eat a combination of different foods, including fruit, vegetables, legumes, nuts and whole grains. A...

  View more
Usivute Sigara
Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mapafu yako, uvutaji wa sigara unaweza sababisha matatizo ya...

  View more
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta

Fats consumed should be less than 30% of your total energy intake. This will help prevent unhealthy...

  View more
Kuendesha Gari.
Kuendesha Gari.

Unashauriwa kutokuendesha gari kila siku na wakati mwingine unatakiwa kutembea walau miguu yako na m...

  View more
Epuka ulevi wa Pombe
Epuka ulevi wa Pombe

There is no safe level for drinking alcohol. Consuming alcohol can lead to health problems such...

  View more