Mwanzo / Huduma Zetu / MKURUGENZI MTENDAJI BMH ATETA NA CHAMA CHA MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI TANZANIA

MKURUGENZI MTENDAJI BMH ATETA NA CHAMA CHA MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI TANZANIA

Published on June 16, 2023

Article cover image

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ameeleza ukuaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ndani ya muda mfupi katika mkutano wa chama cha madaktari bingwa wa upasuaji Tanzania  unaofanyika mkoani Dodoma.

Akizungumza na madaktari hao leo katika ukumbi wa St. Gasper Dkt. Chandika amewaeleza jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa ilipoanza na mpaka ilipofikia hivi sasa pamoja na changamoto walizopata kipindi cha nyuma.

"Ukiiangalia BMH sasa unaweza kufikiri ilianza kama ilivyo niwaambie leo haikuwa hivyo kwani tuliazima mpaka wagonjwa ili kufanya uzinduzi wa Hospitali, najivunia kwa kuwa nami ni Daktari Bingwa wa upasuaji na ukuaji wa Hospitali umekuwa mikononi mwangu."

Kwaupande wake Rais wa chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Larry Akoko ameeleza

"Nakupongeza Dkt. Chandika kwa wasilisho zuri na kazi kubwa inayo acha alama katika Hospitali ya Benjamin Mkapa sote ni mashaidi wa hili na kama mwananchi wa kanda ya kati akiamua kwenda Dar kufuata matibabu ni maamuzi yake mwenyewe maana BMH inajibu maswali yote ya matibabu" alisema Dkt. Akoko