Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho wazinduliwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa
Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho wazinduliwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa

WATU wenye tatizo la kisukari cha macho katika Kanda ya Kati sasa hawana sababu ya kusafiri mpaka Dar es Salaam ili kupata matibabu ya ugonjwa huo baada ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kupatiwa na Serikali kifaa cha kupimia ugonjwa huo (Fundus Camera)

Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt. Alphonce Chandika, amesema asilimia 12.5 ya wagonjwa 61 walikutwa na ugonjwa wa kisukari cha macho mwanzoni mwa mwezi Aprili katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

“Wagonjwa walipewa rufaa kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro. Lakini mpango huu sasa utapunguza rufaa za ugonjwa wa kisukari cha macho,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa BMH wakati wa uzinduzi wa Huduma za Macho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)

Uzinduzi huo ulienda sambamba na kukabidhiwa kwa kifaa cha kupimia ugonjwa wa kisukari cha macho kutoka Serikalini. Serikali kwa kushirikiana na wadau, Hospitali ya Raigmore ya nchini Scotland, wameipatia Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kifaa hicho.

Dkt. Chandika ameishukuru Serikali na wadau kwa kuwezesha kupatikana kwa kifaa hicho cha upimaji wa kisukari cha macho, akisema Hospitali ya Benjamin Mkapa imetenga siku ya Jumanne kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye tatizo hilo.

Manager of National Eye Care Programme in the Health Ministry, Dr Bernadetha Shilio, informed that in 2015, the government had conducted an evaluation exercise to find out if diabetic patients get access to eye medication.

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt Bernadetha Shilio, anasema mwaka 2015, Serikali ilifanya tathimini kwa wagonjwa wa Kisukari na huduma za macho kwa wagonjwa walio hatarini kupata kisukari cha macho.

 “Tathimini hii ilionyesha upungufu kwenye utalaamu, vifaa, na vifaa tiba eneo la kutolea huduma za uchunguzi na tiba kwa wagonjwa hawa. Tathimini ilionyesha 30% tu ya wagonjwa wa kisukari kufikiwa na huduma za uchunguzi wa macho,” alisema.

Dkt Shilio anasema kufuatia matkeo ya tathimini hiyo, Serikali iliandaa mwongozo wa Huduma za Macho kwa Wagonjwa wa Kisukari na Huduma za Macho ili kuokoa uoni wa mtu mmoja kupitia uchunguzi wa macho.

“Aidha, uwepo wa Mwongozo wa Huduma za Macho kwa Wagonjwa wa Kisukari ulikuwa ni mojawapo wa shughuli za kimkakati ulioandaliwa kwa ufadhili wa Vision 2020 na Colege of Ophthalmologists for East, Central and Southern Africa,” alisema.

Dkt Shilio alisema kuwa Serikali iliridhia Mwongozo huo na kuuzindua mwaka 2018, akisema kuwa mpaka sasas, nakala laini na ngumu 500 zimesambazwa kwa hospitali za rufaa za Taifa, Kanda na mikoa yote nchini.

“Takwimu kabla ya Mkakati huo kuwepo zilionyesha ongezeko la wagonjwa wanaofanyiwa uchunguzi kutoka pungufu ya 700 hadi kufikia takribani wagonjwa 18,000 kwa mwaka,” aliongeza.

Dondoo za Afya na Habari
Kula Mlo Kamili
Kula Mlo Kamili

Eat a combination of different foods, including fruit, vegetables, legumes, nuts and whole grains. A...

  View more
Usivute Sigara
Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mapafu yako, uvutaji wa sigara unaweza sababisha matatizo ya...

  View more
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta

Fats consumed should be less than 30% of your total energy intake. This will help prevent unhealthy...

  View more
Kuendesha Gari.
Kuendesha Gari.

Unashauriwa kutokuendesha gari kila siku na wakati mwingine unatakiwa kutembea walau miguu yako na m...

  View more
Epuka ulevi wa Pombe
Epuka ulevi wa Pombe

There is no safe level for drinking alcohol. Consuming alcohol can lead to health problems such...

  View more