Mwanzo / Huduma Zetu / SIKU YA MOYO DUNIANI - WATOTO 68 WACHUNGUZWA MOYO BMH

SIKU YA MOYO DUNIANI - WATOTO 68 WACHUNGUZWA MOYO BMH

Published on September 29, 2022

Article cover image

SIKU YA MOYO DUNIANI - WATOTO 68 WACHUNGUZWA MOYO BMH

Wazazi wajitokeza kwa wingi kupeleka watoto kuchunguzwa na kutibiwa magonjwa ya Moyo kwenye kambi ya uchunguzi na matibabu ya Moyo inayoendelea katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Moyo wa Hospitali hiyo wameungana na wenzao kutoka Shirika lisilo la kiserikali la One New Heart Foundation pamoja na wengine kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando kufanya uchunguzi na kutibu watoto wenye matatizo ya Moyo kwa siku 5.

Jumla ya watoto 68 walifanyiwa uchunguzi wa matatizo mbalimbali ya Moyo tangu Septemba 26 hadi kufikia leo Septemba 29, asilimia 91 wamekutwa na matatizo ya Moyo ya kuzaliwa nayo ikiwemo Matundu kwenye Moyo, Matatizo kwenye mishipa ya Moyo na Matatizo kwenye njia ya Moyo.

Hii ni mara ya nne tangu kuanzishwa ushirikiano wa kutoa huduma za Moyo kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Shirika lisilo la kiserikali la One New Heart Foundation, watoto zaidi ya 239 wamefanyiwa uchunguzi ambapo 25 walikutwa na matatizo ya Moyo yenye kuhitaji huduma za kibingwa na Ubingwa bozezi.

Kati ya hao 25, watoto 18 walifanyiwa matibabu ya upasuaji kwa njia ya Matundu kupitia mshipa wa paja kwa kutumia Maabara maalumu ya Uchunguzi na Matibabu ya Moyo (Cath-Lab) iliyopo Hospitalini hapo, ambapo watoto 7 walifanyiwa matibabu ya upasuaji wa kufungua kifua.

Dunia inapoadhimisha siku ya Moyo, Mkuu Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma Dkt. Happy Kusima, anatoa wito kwa watanzania kujikinga dhidi ya maradhi ya Moyo kwa Kufanya Mazoezi, kupunguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi, kucha matumizi ya sigara, kupunguza matumizi ya Pombe, kuchunguza Afya zao mara kwa mara na kwa wagonjwa kufuata maelekezo ya wataalamu.