Mwanzo / Huduma Zetu / MADAKTARI BINGWA KUTOKA BMH WAENDELEA KUTOA MATIBABU KATIKA KAMBI YA KUMUENZI DKT. GEORGE DILUNGA

MADAKTARI BINGWA KUTOKA BMH WAENDELEA KUTOA MATIBABU KATIKA KAMBI YA KUMUENZI DKT. GEORGE DILUNGA

Published on March 12, 2025

Article cover image

Madaktari bingwa kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na ABBOTT FUND Tanzania wanaendelea kutoa huduma za matibabu katika shule ya msingi Ihumwa kama sehemu ya kuendelea kumuenzi aliekua Daktari bingwa wa Magonjwa ya Dharura George Dilunga.

Sambamba na huduma hizo Afisa Ustawi wa Jamii kutoa BMH anaendelea kutoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi hao.

Mpaka sasa wanafunzi zaidi ya 500 wamepata huduma hizi katika shule ya msingi Ihumwa. Kambi hii itatamatishwa Machi 8, 2025 katika kituo cha kulelea watoto yatima Kikombo.