Mwanzo / Huduma Zetu / WAPANDIKIZWA BETRI KWENYE MOYO BMH, MADAKTARI 70 WAKIPEWA MAFUNZO

WAPANDIKIZWA BETRI KWENYE MOYO BMH, MADAKTARI 70 WAKIPEWA MAFUNZO

Published on December 01, 2023

Article cover image

Wagonjwa  3 wamenufaika na huduma ya kupandikizwa Betri ya kwenye Moyo katika  kambi ya matibabu ya Moyo na Mafunzo ya kubaini wagonjwa wenye kuhitaji huduma ya kupandikizwa Betri ya kwenye  Moyo iliyofanyika  kwa siku  5 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma. 

Kambi hiyo iliyoendeshwa na Dkt. Raul Garillo, Bingwa wa Moyo na Upandikizaji wa Betri kwenye Moyo kutoka Agentina kwa kushirikiana na timu ya wazawa inayoongozwa na Dkt. John Meda bingwa wa Magonjwa ya Moyo BMH na Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dodoma, iliwanufaisha madaktari 70 kutoka kote nchini  ambapo wagonjwa watatu walipandikizwa Betri kwenye Moyo na Afya zao zimeimarika. 

Dkt. Meda amesema kuwa wenye kuhitaji kupandikizwa betri ya kwenye Moyo ni mgonjwa ambaye umeme hauzalishwi vema katika betri yake ya asili hali inayosababisha mapigo yake ya moyo kushuka chini ya kiwango. 

Dkt. Meda ametaja Umri na Magonjwa ya Moyo ya  muda mrefu kuwa vyanzo vya tatizo la  umeme wa asili kushindwa kuzalisha na kusababisha mapigo ya Moyo kushuka chini ya Kiwango.