WATOTO 13 KUTIBIWA MOYO BMH
WATOTO 13 KUTIBIWA MOYO BMH

WATOTO 13 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO BMH

Septemba 26, 2022. Dodoma

Na Raymond Mtani.

Kambi ya uchunguzi na  matibabu ya Moyo kwa watoto imeanza leo Septemba 26 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, ikishirikisha  Madaktari Bingwa Bobezi wa Moyo wa Hospitali hiyo, wadau kutoka Shirika  la One New Heart Foundation na  kutoka nchini Marekani.

Jumla ya Watoto 13 wanatarajiwa kufanyiwa matibabu ya moyo katika kambi hiyo maalumu kuanzia leo, Jumatatu hadi Ijumaa.

Dkt. Rehema Yona, Daktari Bingwa wa Afya ya Watoto amesema kuwa hadi kufikia asubuhi ya leo, watoto 11 wamelazwa kwa ajili ya maandalizi ya matibabu ya Moyo.

“Baadhi watafanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na wengine watafanyiwa upasuaji wa matundu madogo kupitia njia ya mshipa wa paja katika maabara yetu maalumu ya Uchunguzi na Matibau ya Moyo (Cath-Lab)” Amesema Dkt. Rehema.

Watoto hao 13 wanaotarajiwa kupatiwa matibabu, walikutwa na matundu kwenye Moyo, matatizo katika mishipa na milango ya Moyo.

Jopo la wataalamu 22 likijumuisha Madaktari Bingwa Bobezi, Wauguzi na Wataalmu mbalimbali wa Moyo kutoka nchini Marekani tayari limewasili kuungana na wenzao wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando katika kambi hiyo maalumu ya siku 5 kufanya uchunguzi na matibabu ya Moyo kwa watoto kuanzia leo Septemba 26 hadi 30.

Kwa siku zote tano, kambi hiyo itaendelea kufanya uchunguzi wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Hospitalini  hapo ili kuwaweka katika mpango wa matibabu katika kambi itakayofuata.  

Hii ni mara ya pili kwa kambi ya uchunguzi na matibabu ya Moyo kwa watoto kufanyika kwa ushirikiano baina ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Shirika la One New Heart Foundation.

 

Dondoo za Afya na Habari
Kula Mlo Kamili
Kula Mlo Kamili

Eat a combination of different foods, including fruit, vegetables, legumes, nuts and whole grains. A...

  View more
Usivute Sigara
Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mapafu yako, uvutaji wa sigara unaweza sababisha matatizo ya...

  View more
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta
Punguza Vyakula vyenye mafuta mafuta

Fats consumed should be less than 30% of your total energy intake. This will help prevent unhealthy...

  View more
Kuendesha Gari.
Kuendesha Gari.

Unashauriwa kutokuendesha gari kila siku na wakati mwingine unatakiwa kutembea walau miguu yako na m...

  View more
Epuka ulevi wa Pombe
Epuka ulevi wa Pombe

There is no safe level for drinking alcohol. Consuming alcohol can lead to health problems such...

  View more