Mwanzo / Huduma Zetu / WATOTO WANNE WALIOPANDIKIZWA ULOTO BMH WAMEPONA KABISA SIKOSELI-UMMY

WATOTO WANNE WALIOPANDIKIZWA ULOTO BMH WAMEPONA KABISA SIKOSELI-UMMY

Published on May 14, 2024

Article cover image

Watoto wanne waliopandikizwa uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wamepona kabisa ugonjwa wa sikoseli, amesema Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa Fedha wa 2024-2025 mapema leo bungeni, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema vipimo vimethibisha kuwa watoto hao wanne ambao ni wa kwanza kupandikizwa uloto BMH wamepona kabisa sikoseli.

"Watoto wanne (4) waliopandikizwa uloto Hospitali ya Benjamin Mkapa( BMH) wamepona kabisa siko seli. Dkt Alphonce Chandika (Mkurugenzi Mtendaji wa BMH) na timu yako hongereni sana," amesema Mhe Waziri.

Upandikizaji uloto ni matibabu ya sikoseli yanayotolewa na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) pekee katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Mhe. Waziri ameongeza kuwa BMH pia wameanzisha huduma ya upandikizaji wa mimba kitaalamu IVF.

"Hivyo, wakina mama wenye changamoto ya kubeba mimba sasa suluhisho limepatikana," amesema Mhe Waziri.