Mwanzo / Huduma Zetu / WATUMISHI BMH KUCHANGIA DAMU

WATUMISHI BMH KUCHANGIA DAMU

Published on June 13, 2023

Article cover image

Kuelekea Juni 14 siku ya kuchangia damu duniani baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kutoka Idara ya Maabara wamejitokeza kuchangia damu kama hamasa kwa watumishi wengine na watanzania kwa ujumla.

Kucy kabaja Mkuu wa kitengo cha damu salama kutoka BMH ameeleza kuwa maadhimisho ya siku ya kuchangia damu kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma.

“Maadhimisho haya yatafanyika Juni 14 mkoania Dodoma katika ofisi ya damu salama kanda ya kati na kauli mbiu yetu mwaka huu ni changia damu, changia mazao ya damu, changia mara nyingi zaidi,” alisema Kucy.

Vile vile Kucy ameainisha sifa za mtu anaeweza kuchangia damu.

“Mchangiaji yoyote anatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 18-65, mwenye uzito kuanzia kilo 50, tunaangalia pia uwingi wa damu na kama mtu ana matatizo sugu,” aliongeza Kucy

Ndugu Kucy ameeleza kuwa baada ya kuchangia damu mchangia haruhusiwi kufanya kazi yoyote ngumu itakayochosha mwili ndani ya masaa nane na anatakiwa kunywa maji mengi.

Hata hivyo Kucy amesisitiza kwamba hakuna madhara yoyote yanayoweza kumpata mtu baada ya uchangiaji damu endapo amekidhi vigezo.

Katika hatua nyingine Kaimu Meneja Maabara wa BMH Fred Francis ambae pia ni mmoja wa wachangiaji ameeleza kuwa Idara yake imechangia damu leo ili kuhamasisha watumishi wengine wa BMH kuchangia pia.

“Hii sio mara ya kwanza kwa Idara ya Maabara kuchangia damu ila leo tumefanya hivi kwani tunaelekea kwenye kilele cha maadhisho ya siku ya kuchangia damu duniani Juni 14 na pia kuhamasisha watumishi wenzetu wa BMH kuchangia damu kwani ni moja wapo ya sehemu ya jamii inayotuzunguka,” alieleza Fred Kaimu Meneja Maabara BMH

Faida moja wapo ya kuchangia damu ni kuwa mchangiaji atapata kadi ya uanachama itakayomsaidia yeye na ndugu wa karibu kupata damu kwa uharaka pindi wapatapo tatizo.