Mwanzo / Kurasa / Magonjwa ya Damu

Magonjwa ya Damu

Published on August 12, 2022

Idara ya magonjwa ya damu ilianzishwa April 2018 ikiwa na mtumishi mmoja. Idara ilikuwa ikiona wagonjwa wawili hadi watatu kwa siku.

Idara ilianza na huduma ya ushauri wa kitaalamu (expert consultation) kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa damu kama wagonjwa wa seli mundu, damu kushindwa kuganda (hemophilia) na saratani ya damu.

Kwasasa idara inatoa huduma ya vipimo vya kibingwa kwenye magonjwa yanayoletelezwa upungufu wa damu (bone marrow aspiration and trephine biopsy procedures).

Pia idara inatoa huduma ya kina ya ugonjwa wa seli mundu (comprehensive sickle cell disease care), huduma ya kuzuia mgando wa damu (anti-coagulation clinic/care), kliniki ya hematolojia (general hematology clinic), huduma ya kubadilisha damu (exchange transfusion) na upandikizaji uloto (born marrow transplantation).

Kwa sasa idara inaona wagonjwa 20 kwa siku na ina wataalamu wa magonjwa ya damu wawili, nesi mmoja na medical attendants wawili. Idara inafanya kliniki siku za Jumatatu na Alhamisi, na hufanya vipimo siku za ijumaa.