Mwanzo / Kurasa / Kliniki ya Magonjwa ya Damu

Kliniki ya Magonjwa ya Damu

Published on August 12, 2022

Kliniki ya magonjwa ya Damu  inatoa huduma ya ushauri wa kitaalamu (expert consultation) kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa damu kama wagonjwa wa seli mundu, damu kushindwa kuganda (hemophilia) na saratani ya damu.

Kwasasa Kliniki hii inatoa huduma ya vipimo vya kibingwa kwenye magonjwa yanayoletelezwa upungufu wa damu (bone marrow aspiration and trephine biopsy procedures).

Pia kliniki inatoa huduma ya kina ya ugonjwa wa seli mundu (comprehensive sickle cell disease care), huduma ya kuzuia mgando wa damu (anti-coagulation clinic/care), kliniki ya hematolojia (general hematology clinic), huduma ya kubadilisha damu (exchange transfusion) na upandikizaji uloto (born marrow transplantation).

Madaktari huona wagonjwa siku za Jumatatu na Alhamisi, na hufanya vipimo siku za ijumaa.