Medical Tourism
Published on June 27, 2025

UTALII WA MATIBABU NA HUDUMA MKOBA
Hospitali ya Benjamin Mkapa kama Hospitali ya Kibingwa na Bingwa Maalum ina jukumu la kukuza huduma za afya kupitia ujenzi wa uwezo kwa vituo vya afya nchini Tanzania pamoja na kutoa huduma za kibingwa na bingwa maalum kwa jamii ya Kitanzania.
Katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021, hospitali imefanikiwa kutekeleza jumla ya programu 72 za uhamasishaji wa afya (outreach) katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Katavi, Manyara, Iringa, Njombe, Tabora na Zanzibar, ambapo jumla ya wagonjwa 18,580 walihudumiwa.
Hospitali pia imekuwa kinara katika kuendeleza utalii wa matibabu, kwa kushiriki katika kuhamasisha huduma za kibingwa na bingwa maalum zinazotolewa na hospitali kwa nchi nyingine barani Afrika kama vile Uganda, Rwanda, Burundi na Visiwa vya Comoro, pamoja na nchi za kimataifa kama Uturuki, Marekani, Uholanzi, Austria na nchi za Mashariki ya Kati (ikiwemo Kuwait).