Mwanzo / Kurasa / Kliniki ya Mfumo wa Mishipa ya Fahamu na Mifupa

Kliniki ya Mfumo wa Mishipa ya Fahamu na Mifupa

Published on August 12, 2022

Kliniki ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, inatoa huduma za Upasuaji wa Mifupa (Trauma), kuona Wagonjwa wa nje na wa ndani (in and out patient), ambapo inatoa huduma kila siku kwa wagonjwa wa nje na wa ndani. Kliniki ya Mifupa na Mishipa ya fahamu pia inatoa huduma kama vile Upasuaji wa kubadili Nyonga na Magoti, Upasuaji wa Matundu (arthroscopy).

Kliniki ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, kwa sasa pia inatoa huduma ya upasuaji wa dharura wa Ubongo na uti wa Mgongo, kutokana na uwezo mkubwa wa kliniki ya Mifupa na Mishipa ya fahamu pia inafanya Upasuaji Mkubwa wa Kibingwa wa kutoa vimbe katika Ubongo na Uti wa Mgongo, Upasuaji wa Mgongo kwa waliovunjika kwa kutumia vipandikizi vya kuunga.

Kliniki ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, inatoa huduma ya upasuaji wa matatizo ya Ubongo kwa kutumia kamera inayopita kwenye matundu madogo (endoscopic surgery) mfano, kwa watoto wenye vichwa vikubwa, na vimbe katika ubongo.