Mwanzo / Kurasa / Fiziotherapia

Fiziotherapia

Published on August 12, 2022

Idara ya physiotherapy ilianza mwaka 2018 ikiwa na mtaalamu mmoja na ilikuwa ikitoa huduma katika kliniki ya mifupa siku ya jumatatu, jumatano na ijumaa. Wakati idara hii inaanza walikuwa na vyumba viwili na hakukuwa na vifaa vya kutosha.

Baada ya muda idara ikaongezewa watumishi wawili na mpaka sasa ina watumishi watano ambapo watatu ni physiotherapists, nesi mmoja na medical attendant moja.

Mwaka 2021 idara ilipewa eneo lake la kutolea huduma na hapo idadi ya wagonjwa ilianza kuongezeka ambapo awali walikuwa wakiona wagonjwa 8 hadi 12 kwa siku lakini kwa sasa idara inahudumia hadi wagonja 71 kwa siku.

Idara inatoa huduma za tiba ya utengemavu kwa watoto wenye ulemavu na utindio wa ubongo, watu wazima wenye kiharusi, mgongo, walioumia na kuumiza uti wa mgongo na shida za muda mrefu.

Idara inaeneo maalum kwaajili ya watoto, sehemu ya mazoezi na eneo maalum kwaajili ya viongozi pindi wanapoenda kupata matibabu.

Idara ina vifaa vya kisasa ambavyo vinasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma na wagonjwa kupona haraka.