Mwanzo / Kurasa / Kliniki ya Mfumo wa Mkojo na jinsia ya Kiume

Kliniki ya Mfumo wa Mkojo na jinsia ya Kiume

Published on August 12, 2022

Kliniki ya Mfumo wa mkojo na Jinsia ya Kiume inatoa huduma za endoscopic (upasuaji wa matundu) kwa wagonjwa wenye tezi dume, kansa zakibofu, upandikizaji wa figo na upondaji wa mawe kwa kutumia miale midogo midogo.

Kwa upande mwingine kliniki hii inatoa huduma kwa watoto wenye tatizo la jinsia tata, kansa ya figo na wenye tatizo la njia za mkojo na pia kwa wanawake wanaopata matatizo kipindi cha upasuaji.

Kliniki hii inatoa huduma maalum kwa viongozi siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi.

Katika kliniki ya urolojia idadi ya wagonjwa imeongezeka ukilinganisha na hapo awali ambapo sasa hivi kliniki ina hudumia wagonjwa 70 hadi 90 kwa siku kutoka mikoa mbalimbali.