Cath lab Service
Published on October 21, 2024
Maabara ya "catheterization" (Cath Lab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa inawawezesha timu yetu ya Madaktari, wauguzi na wataalamu wa teknolojia kufanya taratibu (procedures) za uchunguzi na matibabu zinazohusiana na moyo na mfumo wa mishipa ya damu. Taratibu (Procedures) hizi mara nyingi ni za kuvamia (invasive) kidogo na zinahusisha matumizi ya Catheters (thin, flexible tubes) zinazowekwa mwilini kupitia mishipa ya damu.
Tunayo uzoefu katika kutambua na kutibu hali kama:
- Coronary artery disease (Vizuizi katika mishipa ya damu ya moyo)
- Angioplasty and stent placement (Kufungua mishipa ya damu iliyojaa au iliyoziba)
- Electrophysiology studies Kugundua na kutibu arrhythmias (matatizo ya mapigo ya moyo)
- Valvuloplasty (Kurekebisha au kubadilisha valvu za moyo)
- Cardiac catheterization (Kupima shinikizo na mtiririko katika moyo)