Executive
Published on November 13, 2024

KLINIKI YA "EXECUTIVE"
Kliniki ya Executive ipo ghorofa ya kwanza katika jengo la awamu ya kwanza. Kliniki hii imeundwa kutoa huduma za afya za ubora wa hali ya juu kwa wageni na wateja wanaohitaji huduma za kitaalamu kwa wakati na kwa hadhi ya juu.
Kliniki hii iko chini ya uongozi wa Daktari Bingwa wa Dharura (EMD) na hufanya kazi siku zote za wiki, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni siku za kazi (Jumatatu–Ijumaa), na saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana siku za mwisho wa wiki (Jumamosi–Jumapili).
Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine waliobobea, wenye mafunzo ya hali ya juu na uzoefu mkubwa, huhudumia mgonjwa mmoja kwa wakati mmoja, wakizingatia mahitaji binafsi ya kila mmoja.
Kliniki hii ina vifaa vya kisasa kabisa, mifumo ya kielektroniki ya kuhifadhi taarifa za afya na mazingira rafiki kwa wagonjwa pamoja na familia zao. Kliniki ina:
- Vyumba viwili vya ushauri (Consultation)
- Chumba cha utaratibu wa matibabu (Procedure Room)
- Vyumba viwili vya kungojea
- Chumba cha uangalizi (Observation Room)
- Vyoo vilivyo safi na vya kisasa
Sehemu ya kungojea ina burudani na vinywaji baridi ili kuleta hali ya faraja na utulivu, huku ukiruhusiwa kuendelea na kazi zako au kusubiri kwa subira hatua inayofuata.
Huduma na Maelekezo Muhimu:
- Wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa siku hiyo hiyo (Day Surgery), uchunguzi wa moyo (Cardiac Evaluation) au kulazwa, watasindikizwa na kuhudumiwa kulingana na mpangilio wa huduma wa vitengo husika.
- Wagonjwa watakao kuwa wakisubiri huduma nyingine watatakiwa kuketi kwenye chumba cha kungojea, ambako watapewa vinywaji na vitafunwa kulingana na chaguo na mapendekezo ya daktari.
- Wakati wa kusubiri, kila mgonjwa atapewa kipeperushi cha mwongozo wa huduma, kitakachompa maelezo ya njia ya huduma na matarajio yake.
- Kwa maswali, maoni au miadi, tafadhali piga simu 0734331099 au tuma barua pepe kupitia info@bmh.or.tz
- Kwa lengo la kuboresha huduma na kuendeleza ubora, wagonjwa wataombwa kujaza dodoso fupi la maoni ili kuelezea kiwango ambacho hospitali imekidhi matarajio yao. Maoni haya hutolewa kwa hiari na yanathaminiwa sana.
Tunawatakia uzoefu wa kipekee na uponaji wa haraka ukiwa katika Kliniki yetu ya Executive. Faragha yako, usalama na afya yako ni kipaumbele chetu. Tuna utaalamu, uzoefu na vifaa vya kisasa vinavyotuwezesha kukuhudumia wewe na familia yako kwa njia bora, ya kitaalamu na kwa kutumia sayansi ya kisasa.
Kwa miadi au maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia +255 (0) 735000002